
Rajabu Abdarahman Abdallah amesema kwamba hata Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amejipambanua kwenye amani na yeyote atakayediriki kuchezea amani hatakuwa na mswalia
Mtume.
Mwenyekiti Rajabu Abrahmani Abdallah ameyasema hayo katika Salaam zake za Eid el Fitr kwa Waislamu wote na Wananchi wa Mkoa wa Tanga ikiwa zimesalia siku chache kukamilika kwa Ibada ya funga na kuingia kwenye kusherehekea Sikukuu hiyo ya Eid El Fitr.
Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Tanga alibainisha kuwa Serikali Mkoa wa Tanga ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Balozi Dkt Batilda Salha Burian na kamati yake ya ulinzi na Usalama wamejiimarisha na kwamba anayetaka kuna aje kwa msingi wa utulivu.
Aidha amewasihi wananchi wote hususani waislamu kusherehekea Sikukuu ya Eid El fitri kwa amani na upendo huku akisema kuwa watakaoleta viashiria vya uvunifu wa amani wanapaswa kukemewa bila hofu