Jumapili , 4th Dec , 2022

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu amesema hataki makundi, rushwa wala kukatana kwenye Mkoa wa Dar es Salama na kuwataka wanachama wote wa chama hicho wavunje makundi yao.

Mtevu ameyasema hayo wakati akikabidhiwa ofisi ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam huku akieleza kwamba kazi yake ya kwanza ni kurudisha mshikamano, kurudisha matumaini kwa watu ambao wanasema wao wabaya.

“Kuna watu ilikuwa wanasema wakina Mtevu wabaya, tunataka kuwaonyesha kuwa sisi sio wabaya, tunachotaka ni umoja na mshikamano, Dar es Salaam imezidi kwa migogoro, sitapenda kuona mnagombana.

“Uchaguzi umeisha makundi mvunje, sisi sote ni kitu kimoja, haina maana kugombana, na watakaoendeleza migogoro tutafungia, na msikimbilie msituni tukae humu humu kama kuonyana tuonyane.Watakaobainika kula rushwa tutawafungia, tunataka Dar iliyo safi, na nikikufungia mimi hakuna wa kukufungulia,"amesema.