Kaimu Mkurugenzi wa Hospital hiyo, Blenda Msangi, ametaja matatizo hayo kuwa ni yale yanayoweza kusababisha ulemavu wa kudumu na ambayo iwapo hayatatibiwa katika hatua za awali yanaweza kusababisha ulemavu wa kudumu.
Kwa mujibu wa Msangi, sehemu kubwa ya matatizo ya viungo na mishipa ya fahamu yanaweza kutibika ambapo ameitaka jamii kutowaficha watoto wanaozaliwa na ulemavu na badala yake wawafikishe hospitalini hapo kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalamu.
Msangi ameongeza kuwa zaidi ya wagonjwa laki moja wamekuwa wakihudumiwa na hospital hiyo kila mwaka huku idadi kubwa kati ya hao wakiwa ni watoto wenye matatizo ya mdomo wa sungura, vifundo vya mguu na mtoto wa jicho.
Kwa upande wake muuguzi mkuu kitengo cha macho Bi. Rehema Mahimbu amelitaja tatizo la umasikini katika ngazi ya kaya kuwa ni moja ya vyanzo vinavyochangia ongezeko la magonjwa yaliyotajwa hapo juu.