Jumatatu , 27th Jul , 2015

Zoezi la uandikishwaji katika dafati la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR, imeelezwa linakwenda kwa kusuasua na kuashiria kuwa kwa siku nne zilizobaki tume haitaweza kuwa imekamilisha kuandikisha watu wote ilitarajia.

Wakazi wa Ubungo wakiwa kwenye foleni ya kujiandikisha vitambulisho vya kupiga kura kwa mfumo wa BVR

Mpaka kufikia jumamos Wilaya ya Kinondoni ilikua imeandikusha watu 94 elfu tu huku Wilaya ya ilala ikiwa imeandikisha wa laki 1,57,264 ambao walikuwa wameandikishwa pamoja na kupewa vitambulisho.

Aidha katika maeneo mengi imeonyesha kuwa mashine za BVR bado zina changamto nyingi ikiwa ni pamoja na kuisha chaji kwa haraka kutokana na maeneo wanaoandikishia kukosa umeme hivyo kufunga zoezi kabla ya wakati.

Changamoto nyingine inayolikumba zoezi hilo ni pamoja na mashine kushindwa kufanya kazi kutokuwa na watalaamu wa kutosha kuendesha mashine hizo kunakofanya misururu kuwa mirefu ikiwa ni pamoja na kutokuwepo kwa utaratibu mzuri wa foleni hali inayolalamikiwa na Wananchi wengi.

East Africa Radio ilishudia katika kituo cha Makuburi, Mabibo wananchi wakijitolea magari yao kwa kutumia betri za magari kuwasha mashine hizo ili zoezi hilo liweze kuendelea baada ya kutokuwepo kwa umeme katika maeneo hayo.