Alhamisi , 11th Mei , 2017

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limewatangaza washindi wawili ambao ni Josephine Lemoyan na Pamela Maasay kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) baada ya kuwabwaga wenzao.

Washindi hao walichuana na Ezekia Wenje, Prof. Abdallah Safari, Lawrence Masha na Salum Mwalimu japokuwa Masha na Wenje walionekana kushiriki katika uchaguzi wa awali Aprili 4 mwaka huu ambapo yalipelekwa majina yao pekee na mjadala mkubwa bungeni na mwishowe kupigiwa kura za Hapana.

Kutokana na ushindi huo, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah ameweka hadharani majina yote tisa ya wabunge wa Eala kutoka Tanzania kuwa ni Pamela Maasay, Josephine Lemoyan, Adam Kimbisa, Mohamed Habib Mnyaa, Dk Abdullah Makame, Dk Ngwaru Maghembe, Happiness Legiko, Maryam Ussi Yahya pamoja na Fancy Nkuhi,