Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X taarifa ya yeye kujeruhiwa kwa risasi imewekwa na mweka maudhui wake mtandaoni yaani 'Admin' na tayari amefikishwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Jumanne , 3rd Sep , 2024
Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kwa jina la Bobi Wine amepigwa risasi mguuni na polisi wakati wakirusha mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wake katika eneo la Bulindo nchini humo.