Jumatatu , 23rd Sep , 2019

Benki Kuu ya Tanzania imezitoza faini benki tano za biashara kwa kwenda kinyume na Kuzuia Utakatishwaji wa Fedha Haramu za ya mwaka 2012, ambapo wameshindwa kuhakiki taarifa za utambulisho wa wateja.

Aidha kosa jingine inazozikabili benki hizo ni kutowasilisha taarifa ya miamala yenye kuleta mashaka katika Kitengo cha Kuzuia Fedha Haramu (FIU).

Benki ambazo zimetozwa faini na Benki Kuu ya Tanzania ni African Banking Corporation (T) Limited TSH 145 milioni, Equity Bank (Tanzania) Limited TSH 580 milioni.

I&M Bank (T) Limited wametozwa 655 milioni, UBL Bank (T) Limited TSH 325 milioni
na Benki ya Habib African Bank Limited wametozwa 175 milioni

Aidha Benki Kuu ya Tanzania imezitaka benki hizo kupitia upya taarifa za wateja wao na kuhakikisha, zinakidhi matakwa ya kisheria na kanuni zilizopo za uhakiki wa utambulisho wa wateja.

Pia imezitaka kuwachukulia hatua za kinidhamu, wafanyakazi waliohusika kufanikisha ufunguaji wa akaunti za amana.