Alhamisi , 18th Aug , 2022

Idadi ya vifo vilivyotokana na ajali ya basi la kampuni ya Tanzanite imeongezeka kutoka vifo vinne hadi vitano hii leo. basi hilo lilipata ajali jana Agosti 17, 2022, katika Kijiji cha Mbwasa wilayani Manyoni mkoani Singida wakati likitoka jijini Mwanza kuelekea Dar es Salaam.

Basi la Tanzanite lililopata ajali

Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida ACP. Stella Mutabihirwa, mapema hii leo na kusema gari hilo lilikuwa kwenye mwendo mkali hali iliyopelekea dereva kushindwa kulimudu na ndipo tairi la upande wa kulia lilipopasuka na basi kwenda kugonga tuta lililokuwepo pembezoni mwa barabara.

Kamanda Mutabihirwa, amesema kwamba katika ajali hiyo jumla ya watu 15 wamejeruhiwa katika ajali hiyo na kusema bado madereva wamekuwa wakiendesha kwa mwendo wa hatari bila kuchukua tahadhari, na kuwasihi madereva wafuate sheria za barabarani.