Mhandisi Edwin Ngonyani
Mhandisi Ngonyani ameyasema hayo leo wakati akizindua mkutano wa kwanza ambao umeandaliwa na Tume mpya ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambapo amesema wataalam hao watajadiliana namna gani taaluma hiyo inavyoweza kutumika zaidi kwa faida ya ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.
Ameongeza kuwa Tume hiyo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inatakiwa kuja na sheria kali ambazo zitawabana wale wote ambao wamekuwa na tabia ya kutumia mitandao katika kufanya vitendo viovu badala ya kutumia katika kujiletea maendeleo.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustine Kamuzora amesema sekta ya TEHAMA itazalisha ajira mpya kwa wataalam waliosomea fani hiyo sambamba na kulinda siri za serikali dhidi ya wadukuzi wa mtandao.