Alhamisi , 16th Jun , 2016

Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje CCM ameiambia serikali katika Bunge linaloendelea Dodoma kwamba baada ya mvua kunyesha katika maeneo mengi nchini barabara zimebakia katika hali mbaya na kutopitika na kutaka kauli.

Lubeleje ameyasema hayo alipokuwa akiuliza swali la papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ikiwa leo nisiku ya alhamisi ambapo huwa na kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu na kutaka hatua za serikali za dharuda katika kutatua kero hiyo ambayo ni kikwazo cha shughuli za maendeleo katika maeneo mengi nchini.

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Kassim amesema kwamba serikali imekwishatoa maelekezo kwa TANROADS na mfuko wa barabara ili kushughulikia barabara zote ambazo zimeharibika kipindi cha mvua.

''Jukumu la serikali ni kusisitiza mifuko hii ikarabati barabara ili ziweze kupitika na shughuli ziweze kuendelea kama kawaida''- Amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.