Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa nishati, maji nchini Felix Ngamlagosi akizungumza na waandishi
Akizungumza na wadau wa Mafuta jana Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi mkuu wa Huduma za Nishati na Maji nchini EWURA, Felix Ngamlagosi amesema mwaka 2012 kulikua na mfumo wa uagizaji mafuta wa pamoja ambao kwa kiasi kikubwa ulisaidia kupunguza gharama za uingizaji mafuta nchini na ukusanyaji wa mapato.
Aidha Ngamlagosi ameongeza kuwa mgumo ho utasaidia nchi kushindana vyema kibiashara na bandari za Mombasa ya Kenya, Beira ya Msumbiji na Afrika Kusini na kuliingizia pato taifa kupitia wafanyabiashara wa nje wanaotumia bandari ya Dar es Salaam.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Walaji EWURA CC, Prof. Jamidu Katima amesema ikiwa mafuta yatakuwa yakishushwa katika bandari hiyo kwa bei nafuu ni wazi kuwa gharama za mafuta kwa watumiaji wa mikoa ya jirani na mkoa husika zitakuwa chini.