
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka Jiwe la Msingi Kongani la Viwanda Kwala Pwani, leo tarehe 31 Julai, 2025.
Pia, Rais Samia amezindua Treni ya umeme ya mizigo itakayokuwa ikisafirisha mizigo kati ya Dar es Salaam na Dodoma.
Katika Kongani ya Viwanda Kwala, tayari viwanda saba vinafanya kazi na vitano vikiwa katika hatua za mwisho za ujenzi. Kongani hiyo yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni tatu, imejengwa katika eneo lenye ukubwa wa ekari 2,500.
Aidha, inalenga kuwa na zaidi ya viwanda 200 hatua inayotarajiwa kuimarisha kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sekta ya viwanda nchini. Pia hatua hiyo itaongeza ufanisi wa usafirishaji wa bidhaa kwenda masoko ya ndani na nje ya nchi.
Kwa mujibu wa Mhe. Dkt. Selemani Saidi Jafo, Waziri wa Viwanda na Biashara, mradi huo mkubwa unatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 50,000 za moja kwa moja na ajira zisizo za moja kwa moja zipatazo 150,000 kwa Watanzania. Tayari watu 311 wamekwishapata ajira kupitia shughuli zinazoendelea hapo.
Kwa upande wa bandari kavu ya Kwala, inatarajiwa itakuwa na bandari kavu tisa za nchi jirani zinatumia Tanzania kama lango kuu la kusafirisha bidhaa. Uzinduzi wa Bandari ya Kwala na ubebaji mizigo kupitia treni ya SGR na bandari hiyo utapunguza mrundikano wa mizigo Bandari ya Dar es Salaam kwa asilimia 30. #EastAfricaTV