
Sheikh Luwuchu ametoa agizo hilo wakati alipokutana na viongozi wa dini wa mkoa wa Tanga wakiwemo maaskofu katika kikao maalum cha kuliombea taifa amani hasa kipindi hiki bunge la Katiba likiendelea na mchakato wa rasimu ya pili ya Katiba.
Amesisitiza kwamba ni vema viongozi wa dini na waumini wa dini wakaungana na serikali katika kuhakikisha kwamba amani inadumu na sio wa kwanza kuharibu matakwa ya watanzania ya kuwepo kwa amani na utulivu hapa nchini.