Moja ya maadhimisho ya Maulid
Katika taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa baraza hilo, Mohammed Khamis Said, kwa vyombo vya habari, BAKWATA imetangaza kuwa mwezi uliandama usiku wa Jumanne, tarehe 30 SAFAR 1441H sawa na Oktoba 29, 2019, hivyo leo ni mwezi mosi (tarehe 01 RABIUL AWWAL) sawa na Oktoba 30, 2019.
Maulid ya kitaifa yataadhimishwa usiku wa Jumamosi, mwezi 11 RABIUL AWWAL 1441H sawa na Novemba 9, 2019 katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza na Baraza la Maulid litafanyika Jumapili Novemba 10, ambayo ndiyo itakuwa siku ya mapumziko kitaifa. Baraza litaanza saa 9:00 Alasiri katika ukumbi wa Benki Kuu (BOT), Kapripoint, Mwanza.
Soma zaidi taarifa hii hapa chini.