Mchungaji Ambilikile Mwaisapile maarufu Babu wa Loliondo
Babu wa Loliondo ameyabainisha hayo wakati akizungumza na EATV, na kusema kuwa licha ya idadi ya watu wanaofika kijijini hapo kupungua kwa ajili ya kunywa kikombe chake, lakini huduma yake bado inaendelea.
"Nimeelezwa na Mungu habari ya tetemeko kubwa, ambalo linakuja na halina madhara, hakuna mtu atakayekufa wala nyumba kuanguka, hata likija usiku mvua inanyesha watu wasikimbie kwenda nje litatikisa masaa manne, kuanzi saa 6:00 na litakata saa 10:00 usiku" amesema Babu wa Loliondo.
Hadi sasa ni takribani miaka tisa imepita, tangu Babu wa Loliondo alipoibua kikombe ambacho kilielezwa, kuponya magonjwa mbalimbali na kiliwavuta watu wengi kutoka nchi mbalimbali.
