Mh. Paul Makonda amesema hayo leo Mei 17, 2018 wakati wa alipokuwa anatoa salamu kwa Rais Magufuli katika sherehe za ufunguzi wa kituo cha uwekezaji cha SUMA JKT Mgulani Jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa alizaliwa na kulelewa katika kambi za jeshi
“Nikunong’oneze mheshimiwa Rais, mimi nimezaliwa kambini na baba yangu ni miongoni mwa askari waliopigana vita nyingi ikiwemo vita ya Uganda na mpaka ulemavu wake wa mguu ni kutokana na kazi ya kuipigania Tanzania” amesema Makonda
Makonda aliongeza kuwa kutokana na kulelewa katika kambi za jeshi imemsaidia kupata ujasiri wa kuongoza mkoa wa Dar es salaam wenye changamoto nyingi na kuweza kufanya kuwa Jiji la raha Tanzania.
Katika tukio hilo, Rais Dkt Magufuli alizindua kituo cha uwekezaji cha SUMA-JKT ambacho ndani yake kuna kiwanda cha Ushonaji, Maji, Chuo cha Ufundi Stadi na Ukumbi wa Mikutano.