
Kamanda Polisi mkoani Mwanza, Jumanne Murilo
Tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Kisesa A na kuzua simanzi kubwa kwa familia na majirani kufuatia kumpoteza mtoto, Agness Anthony mwenye umri wa miaka 8 anayesoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Bujora ambaye mwili wake umekutwa katika eneo la michezo.
Neema Petro ambaye ni mama mzazi wa mtoto Agness akilia kwa uchungu wa tukio hilo amesema kuwa hakuwa na namba na mumewe, hivyo alipata taarifa kuwa mwanaye ni mgonjwa kupitia kwa majirani ndipo alipofuatilia na kukuta amefariki.
Mwenykiti wa Kijiji cha Kisesa A, Lucas Magembe amesema taarifa hizo alizipata kutoka kwa wanakijiji huku Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la KIVULINI, Yassin Ally akiitaka jamii kutonyamazia vitendo hivyo vya kikatili.
Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amethibitisha jeshi hilo kumshikilia baba wa mtoto anaedaiwa kuhusika na kifo hicho huku mwili wa mtoto Agness ukiwa umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa Bugando ukifanyiwa uchunguzi zaidi.