
Mbunge wa Saboti, Caleb Amisi amesema kuwa ni rahisi sana kumuondoa Ruto madarakani kwa sababu alishinda kwa kura chache katika uchaguzi
Kwa upande wa Kiongozi wa Azimio Raila Odinga amewataka wananchi kuwa na angalizo na serikali ya Kenya Kwanza huku akisema muswada wa fedha 2023 utakuwa na athari kubwa kwa wananchi na hivyo wanafaa kuukataa mara moja kwa kususia kulipa ushuru.
“Tuliwaambia punda amechoka Hawakutuskiza. Wamezidi kuwekelea mizigo punda mgongoni. Sasa wakati umefika punda sasa awapige mateke"-Amesema Raila.