Jumanne , 6th Jan , 2015

Mkazi wa wilayani moshi mkoani kilimanjaro aliyekuwa akiishi Songea kwa shughuli za kibiashara Bw. Emmanuel Moshi amemuua mfanyabiashara mwenzake aitwaye Didas Alfonce kwa kumkata na shoka kichwani na kisha mwenyewe kujinyonga.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma ACP Mihayo Msikhela

Taarifa zinadai kwamba, Moshi alifikia hatua hiyo baada ya kudhulumiwa shilingi milioni 87.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma ACP Mihayo Msikhela amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema chanzo cha tukio hilo ni wafanyabiashara hao kudhulumiana fedha za biashara za mbao walizopata.

Kamanda mihayo amesema kuwa marehemu ameacha ujumbe wa kurasa nne unaoeleza sababu ya yeye kuua na kisha kujiua.

Katika ujumbe wake kamanda Mihayo anasema marehemu Moshi ametaja fedha alizokuwa akimdai mtu aliyemuua kiasi cha shilingi milioni 87.

Pia marehemu Moshi ameandika namba zake za simu kwa mawasiliano katika bahasha aliyowekea ujumbe huo.