
Taarifa za kukamatwa kwa mwanafunzi huyo ambaye pia ni kiongozi kwenye serikali ya wanafunzi ndg. Kumbusho Dawson zimethibitishwa na Makamu wa Rais (Daruso) Bi Anastazia Anthony ambaye amesema "Ni kweli na kwa sasa ndiyo anapelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay. Asubuhi wanahabari walikuwepo hapa na hata watu wa TBA walikuwepo lakini baada ya kuondoka na yeye ndyo akaja kukamatwa"
Kwa mara ya kwanza na Mbunge Heche aliripoti habari hii akisema kwamba "Nimeambiwa kiongozi wa serikali ya wanafunzi (Daruso) Kumbusho Dawson aliyeripoti nyufa kwenye majengo ya hostel za chuo amekamatwa na polisi!
Hata hivyo sababu za kukamatwa kwake bado hazijajulikana.
Endelea kukaa karibu na wwe.eatv.tv huu kwa habari zaidi