Jumanne , 14th Jun , 2016

Mratibu wa Kitengo cha Selimundu wa Chuo cha Tiba Muhimbili, Dk. Deogratius Soka amesema kuwa asilimia 15 ya Watanzania wako hatarini kupata watoto wenye tatizo la Selimundu kufuatia kubeba vinasaba vya ugonjwa huo bila ya wao kujua.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuelekea siku ya maadhimisho ya Selimundu inayoadhimishwa tarehe 17 mwezi Juni mwaka huu, Dk. Soka amesema kuna haja ya kuhamasisha watu kupima afya zao kabla ya kuamua kupata watoto kwani tatizo hilo litaongezeka zaidi katika jamii.

Aidha, Dkt. Soka ametoa wito kwa serikali kuangalia jinsi ya kuharakisha kupima vipimo kwa Watanzania ili wananchi waweze kujua afya zao na kufanya maamuzi kabla ya kuanzisha familia