Ijumaa , 5th Aug , 2016

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mrisho Gambo,amesema kuwa ofisi yake itaunda kikosi kazi cha kufuatilia wanafunzi hewa katika shule za msingi na sekondari ili kubaini iwapo kuna tatizo hilo na kuchukua hatua za kisheria.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mrisho Gambo,

Kufuatia Agizo la Raisi John Pombe Magufuli kuwaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kufuatilia baadhi ya Wakuu wa shule kuweka idadi kubwa ya wanafunzi hewa ili waweze kupata ruzuku kubwa kutoka serikalini.

Mrisho Gambo akizungumza na Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Wenyeviti katika kikao kazi amesema kuwa kikosi hicho kitaanza kufanya kazi yake mapema na iwapo tatizo hilo likibainika hatua za kisheria na kinidhamu zitachukuliwa hivyo amewataka Wakuu hao kuepuka udanganyifu wa namna hiyo.

Kwa upande wao Mwenyeviti wa Bodi za Shule Eska Msuya wa shule ya Mkombozi Amesema kuwa Licha ya serikali kutoa waraka wa elimu bure bado kuna changamoto ya Walinzi wa shule kukosa mishahara yao na kujikuta wakiishi katika hali ngumu za maisha hivyo wameiomba serikali ijumuishe mishahara ya walinzi katika ruzuku wanazopeleka mashuleni.

Mwenyekiti wa Shule ya Msingi Meru Shija Richard amesema kuwa shule zenye vitengo maalumu vya walemavu wamekua hawapati mafungu maalumu ya kukidhi mahitaji yao muhimu hivyo wameiomba serikali kulikumbuka kundi hilo Pamoja na kujumuisha bili za maji na umeme.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mrisho Gambo,