Jumatatu , 27th Nov , 2023

Mwanamke mwenye umri wa miaka 50 mkazi wa kijiji cha Kilugala kilichopo kata ya Nhobora wilayani Itilima mkoani Simiyu amejeruhiwa kwa kukatwa na panga na mtu asiyejulikana   maeneo ya kichwani na kwenye vidole vya mikono na kusababisha vidole viwili kukatika

Tukio hilo limetokea nyumbani kwa mwanamke huyu ambaye alikuwa na mtoto wake mdogo ambapo hakuweza kumtambua mwanaume aliyemkata na panga 

 "Tulikuwa ndani tu nilikaa nikawashiwa tochi usoni nikaanzia kupigwa mapanga ilikuwa ni saa mbili nikapiga yowe sasa watu wakaja nilikuwa nakaa na katoto kangu kadogo sasa kalikimbia kwenda kwenye majirani kwenda kuwaambia kalikuwa kanalia sana kanapiga yowe majirani wakaja sasa kunisaidia" Ngw'Anza John, Majeruhi 
Sasa tukio hili nikauliza lilikuwa linakuwakuwaje nikamkuta aliyekatwa mapanga nilimkuta kwenye  hospitali" ameeleza Nsiya John  ambaye ni Dada wa majeruhi.

Jamii inashauriwa kuhakikisha kabla ya kukaribisha mgeni taarifa zake zifike kwenye uongozi wa kijiji huku serikali ikiombwa kutoa ulinzi ikiwa ni sambamba na kumuamisha mama huyo mara baada ya kutoka hospitalini.

"Matukio haya ni mabaya ila wananchi sasa hivi nimewaambia wananchi wakae step (standby) na kuangalia mgeni atakayekuja atoe taarifa" ameeleza  Maduhu Kome ambaye ni Mwenyekiti wa kijiji cha Kilugala.

"Kwa kweli yule mama kwanza  makusudio ilikuwa ni kuua ila MUNGU amesaidia yule mama amepona tunakemea sana hilo tukio lililofanyika kwenye kata yangu sijafurahishwa mimi ni mama na aliyekatwa ni mama na yule mama ni nguvu kazi ya wanawake wenzangu yule mama alikuwa anaisaidia familia yake alikuwa akilima analea watoto anapikia watoto anaangalia wajukuu lakini kwa hali iliyompata mama kweli inasikitisha sisi wanawake imetusikitisha sana niiombe tu serikali yule mama akipona umpeleke ikamhifadhi sehemu nyingine maana yake wale waliondoka na simu  yake walipokuwa wakipigiwa walikuwa wanasema kwamba bado tunarudi kwenye kiporo chetu kama kuna sehemu ya kumhifadhi imsaidie yule mama ili kumsaidia" ameeleza Mbuke Ndaki, Diwani wa kata ya Nhobora
Tayari mwanamke huyo amefikishwa hospitalini kwaajili ya kupatiwa matibabu huku jeshi la polisi likitoa taarifa ya tukio hilo 

"Tunakiri tulipokea majeruhi alikuwa na majeraha mbalimbali mikononi na kichwani na alipatiwa matibabu hali yake kwasasa anaendelea vizuri na yupo wodini" Dkt Rosemary Mushi, Mganga Mfawidhi wa hospitali ya halmashauri ya mji wa Bariadi