Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shanna
Taarifa hiyo imetolewa leo Machi 12, 2020 na Kamanda wa Polisi mkoani humo, Jonathan Shanna, na kusema mtuhumiwa huyo aliyejulikana kwa jina la Mkami Shirima, alimpiga binti huyo na kisha kumfungia ndani kwa siku mbili, ambapo baadaye alizidiwa na kumkimbiza hospitali na ndipo mauti yalikomkuta.
"Marehemu alifariki Dunia Machi 9, katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake, tumemhoji mtuhumiwa kwa kina na amekiri, upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kesho Machi 13, 2020, atafikishwa mahakamani" amesema ACP Shanna.
Aidha ACP Shanna amesema kuwa mwili wa marehemu umesafirishwa leo, kwenda mkoani Singida kwa ajili ya mazishi.

