Jumatatu , 4th Apr , 2022

Jeshi la polisi Mkoani Mtwara, linamshikilia Shaibu Kuselela 58, mkazi wa kijiji cha Lipalwe Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara, kwa tuhuma za kumuua mkewe kisha  kumzika shambani.

Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mtwara ACP Nicodemus Katembo

Akizungumza na waandishi wa habari, kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo, ACP Nicodemus Katembo amesema ni mara ya pili kwa mtuhumiwa kutenda kosa la mauaji.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi limekamata pikipiki mia 300, na kutoa onyo kwa watenda makosa mbalimbali na kutoa onyo kwa waendesha pikipiki maarufu kama  bodaboda kufuata sheria za usalama barabara.