Jumanne , 17th Mei , 2022

Mwanamke mmoja nchini Nigeria katika jimbo la Kaduna aitwaye Halima Yunusa, amempeleka baba wa mpenzi wake katika Mahakama ya Kiislamu nchini humo baada ya Baba huyo kumkataa na kutaka asiolewe na mtoto wake Bashir Yusuf.

Nyundo ya Mahakama

Taarifa zimeeleza kwamba Halima aliieleza Mahakama kuwa anapendana na mpenzi wake Yusuf lakini baba wa mpenzi wake huyo amekuwa ndiyo kikwazo cha wao kuoana.

Baba yake na Halima aitwaye , Ibrahim, aliiambia Mahakama kwamba alikuwa anafahamu kuhusu mapenzi baina ya binti yake na Yusuf, lakini alikuwa hajatimiza vigezo vya kuoa kwani kijana aliagizwa hawapeleke wazazi wake na hakufanya hivyo na alirudi baada ya mwaka mmoja na kuondoka na binti yake.

Baba wa binti huyo aliendelea kueleza kuwa baadaye alikutana na baba yake Yusuf ambaye alimuonya kuwa hatamruhusu Yusuf amuoe binti yake.

Baada ya kusikia hoja za pande zote mbili, Jaji alimuamrisha baba yake Yusuf kumruhusu kijana wake amuoe Halima na iwapo hatofanya hivyo Mahakama itawafungisha ndoa.