Alhamisi , 4th Jul , 2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene ameonya matumizi ya gari ya wagonjwa (ambulance)  iliyotolewa na serikali katika kituo cha afya cha Ipera lisitumike kubeba nyumba ndogo badala yake itumike kwa

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene

itumike kwa ajili ya malengo yaliyokusudiwa.

Pia amesema gari hiyo isitumike  kibiashara kwa kuanza kubeba abiria au mazao bali itumikwe kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa hususani akina mama wajawazito.

Waziri Simbachawene ametoa kauli hiyo leo wakati wa hafla ya kukabidhi gari hiyo mara baada ya kufanya mkutano wa hadhara  katika Kata ya Ipera, Kibakwe iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma ambapo amewataka wananchi wawe walinzi wa gari hiyo.

"Msisitizo wangu gari hii ya wagonjwa ni gari la serikali na ni gari ya wananchi hivyo nitawashangaa kuiona gari hii ikibeba abiria au magunia ya mazao, naombeni kila mmoja wetu awe mlinzi wa gari hii kwani ni yetu sote," amesisitiza Waziri Simbachawene

Amefafanua kuwa azma ya serikali ya kutoa gari hiyo ni kuhakikisha inasaidia kuwafikisha wagonjwa katika hospitali ya Rufaa kwa muda muafaka pale ambapo mgonjwa anapewa  rufaa ya matibabu.