Tukio hilo ni la tatu katika eneo hilo la Pasua kwa mwaka huu la watu kuchukua uamuzi wa kujinyonga kutokana na sababu mbalimbali.
Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia #EATV kuwa marehemu alikutwa asubuhi ya Novemba 14, 2024 akiwa amelala chini baada ya tawi la mti kukatika na kumbwaga chini huku wengine wakidai chanzo cha umauti ni kukata tamaa ya maisha na mahusiano ya kimapenzi.
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro lilifika eneo la tukio baada ya wananchi kutoa taarifa kuhusu kukutwa kwa mwili huo katika eneo la Nelson Mandela ambapo hadi sasa wanaendelea na uchunguzi wa kina kutokana na utata kuwa alijinyonga au alinyongwa na watu wengine.