Jumatano , 31st Jul , 2024

Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania limefanikiwa kumkamata Samwel Mbise (42) mkazi wa Sanawari Jijini Arusha akiwa anafanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni bila ya kuwa na kibali.

Fedha

Akitoa taarifa hiyo leo Julai 31, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo, amebainisha kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa kupitia operesheni ambayo inaendelea iliyoanza Julai 29, 2024 ambapo alikutwa na fedha mbalimbali.

SACP Masejo amefafanua kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa na fedha mbalimbali ambazo ni Dola za Marekani 5,952, Euro 835, Dola za Canada 1,845, Pound 45, Switzerland Franc 20, Dola za Australia 50, Qatar Riyals 05, Pound za Egypt 25, Shilingi za Kenya 38,400/= na Shilingi za Tanzania 52,552,000/= ambazo jumla yake ni fedha za Kitanzania shilingi milioni 75,809,649.