Jumatano , 13th Aug , 2014

Mwanamke mmoja Wilayani Songea mkoani Ruvuma amejitengenezea jeneza kutokana na ugumu wa maisha na kutengwa na ndugu kutokana na ulemavu wake.

Bibi Scholarstika Mhagama pembeni ya jeneza alilotengeneza miaka 2o iliyopita

Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Sholastika Mhagama mwenye umri wa miaka  76 ambaye nimlemavu wa miguu  mkazi wa kijiji cha Lundusi  kata ya Peramiho wilayani Songea mkoani Ruvuma amejichongea jeneza analokaa nalo kwenye nyumba yake  kwa madai ya kutengwa na ndugu zake kutokana na ulemavu wake pamoja na kuchoshwa na shida za dunia.

Hotmix imefunga safari hadi Peramiho na kumfuata mwanamke huyo aliyepata ulemavu akiwa darasa la pili baada ya kuumwa na nyoka hali iliyosababisha kukatwa mguu mmoja.
Mwanamke huyo ambaye pia alifiwa na mumewe na wanae wanne, amesema jeneza hilo alilitengeneza kwa miaka zaidi ya ishirini iliyopita kwa pesa ya kuuza pombe miaka.

Tukio lingine kutokea Songea ni kwamba Siku moja baada ya jengo moja  la ghorofa kuungua moto mjini songea mkoani Ruvuma  watu wawili wamejeruhiwa katika ajali  nyingine ya moto iliyotokea maeneo ya Mfranyaki baada ya nyumba moja mali ya Khalifa Omary  kuungua moto na samani zote za ndani kuteketea.

Vilio na majonzi vilitawala eneo  la tukio  ambapo majeruhi  wawili waliojeruhiwa katika ajali hiyo ambao ni  Cauthery Namahala binti wa miaka kumi na moja na Maria Shaweji binti wa miaka kumi na tano  ambao walizimia kutokana  na moshi wa moto na kukimbizwa hospitali ya mkoa kwa matibabu.

Tukio hilo la ajali ya moto limetokea  ikiwa imepita siku moja baada ya jengo moja la ghorofa  lililoko katikati  ya mji wa Songea kuungua moto.