Miongoni mwa daladala iliyoparamiwa
Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya amekiri kutokea kwa ajali hiyo majira ya mchana wa leo Julai 5, 2023, ambapo amesema wote waliofariki ni wanaume.
Kamanda Mallya amesema ajali hiyo imehusisha lori moja la IT, bajaji, bodaboda na lori lingine ambalo limepata hitilafu kwenye mfumo wa breki na kuyaparamia magari mengine.
Kamanda Malyya amesema majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Mpakani Tunduma Wilayani Momba.