Ijumaa , 20th Feb , 2015

Watu wawili wamefariki dunia na wengine 45 wamejeruhiwa baada ya kutokea ajali mbaya ya barabarani iliyohusisha basi la abiria la Kidia na lori la mizigo katika eneo la Vikonje lililopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Basi la Kidia baada ya kupata ajali iliyosababisha vifo vya watu wawili na 45 kujeruhiwa

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, David Misiime amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo majira ya saa saba mchana wakati dereva wa basi la Kidia alipokuwa akitaka kuyapita magari mengine.

Kamanda Misiime ameyataja magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni basi la Abira lenye namba T 663 AXL aina ya Scania bus lilikua likitokea Dar es Salaam Kwenda Mwanza ambalo iligonga na Lori namba T496 CFG likiwa na tela lenye namba T576 AZX aina ya Scania lililokua likiendeshwa na Fadhili Hamadi Said lilikua likitokea Mwanza kuelekea Dar es Salaam.

Kamanda Masiime aliwataja watu hao wawili waliofariki katika ajali hiyo ni Dereva wa Lori hilo aliyejulikana kwa jina la Fadhili Hamadi Said (36) msukuma mkazi wa Dumila na pia imesababisha kifo cha utingo wa Basi la Kidia aliyejulikana kwa jina la Chogo Chigunda 30 mkazi wa Dar es salaam na kuongeza kuwa ajali hiyo iliyosababisha majeruhi 45 ambao 18 kati yao walitibiwa na kuruhusiwa.

Amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Dereva wa basi aliyetaka ku over-take gari lililombele yake ndipo walipogonga na lori hilo uso kwa uso na kusababisha vifo hivyo.

Kwa upande wake mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Nassor Mzee amekiri kupokea majeruhi 44 wa ajali hiyo ambapo kati ya hao 18 wametibiwa na kuondoka.