Jumamosi , 21st Oct , 2023

Watu 18 wamefariki dunia na wengine 35 wamejuhiwa baada ya basi la kampuni ya Alfa linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Dar es Salaam kugongana na lori la mafuta mali ya kampuni ya GBP

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Undomo kata ya Uchana tarafa ya Nyasa wilaya ya Nzega mkoani Tabora

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku waliofariki ni wanaume 13 na wanawake watano ambapo chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa