
Ndege iliyopata ajali
Ajali hiyo imetokea leo Mei 18, 2023, kufuatia ndege ya shirika la Frankfurt Zoological aina ya Cessna 182 na usajili wa namba 5H-FZS kupata ajali muda mfupi tu baada ya kuruka kutoka kwenye kiwanja kidogo cha Matambwe Selous.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili Dkt Hassan Abbas, imeeleza kuwa, Rubani Shayo pamoja na Mgogolo walifariki papo hapo, huku Askari Mhifadhi Nota, amefariki wakati ndege iliyokuwa ikimuwahisha hospitali kutua katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam
Kufuatia ajali hiyo Rais Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro Adam Malima kufuatia vifo hivyo.
Taarifa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii