Jumanne , 12th Sep , 2023

Mtu mmoja amefariki dunia hii leo Septemba 12, 2023 katika ajali iliyohusisha gari la mwendokasi na bodaboda katika makutano ya mataa ya Lumumba na barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam.

Eneo la ajali

Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wamethibitisha kifo hicho kuwa ni cha dereva bodaboda ambaye alikuwa akitumia barabara ambayo ni maalum kwa ajili ya mabasi hayo.

Aidha undani wa tarifa hiyo utakuja baadaye.