
Mwanaume huyo ambaye alipenda kutambulika kama DK kwa ajili ya kutunza faragha yake ,amesema kuwa alienda katika hospitali hiyo kama mgonjwa kumuona Dokta Samnakay na sio kutumika kama sampuli ya kufundishia.
“Wakati nimelala katika chumba cha kufanyiwa vipimo huku nikiwa mtupu waliingia Wasichana wawili ambao waliniambia kuwa wao kiumri ni wadogo sana kwangu kitu kilichonifanya nishituke sana”, amesema Dk.
Aidha Dk anasema kuwa wakati akichukuliwa vipimo, Daktari aliwauliza maswali Wanafunzi hao wawili kitu kilichomfanya agundue kuwa amegeuzwa sampuli ya kufundishia bila yeye kujua.