Waombolezaji msibani
hicho ambako alikuwa ameshikiliwa na mtendaji wa kijiji hicho kwa tuhuma za kupigana na mwenzake.
Wakizungumza baadhi ya ndugu na wananchi kwenye mazishi ya kijana huyo wamedai kuwa nguvu kubwa ilitumika wakati wakienda kumkamata Frank ambaye sasa ni marehemu baada ya kugombana na mwenzake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkuu wa wilaya ya Ikungi Thomas Apson, amekiri kutokea kwa tukio hilo huku watu watatu wakishikiliwa na Jeshi la Polisi, akiwemo mtendaji wa kijiji hicho Joakimu Mariko Chaba, pamoja na askari wawili wa jeshi la akiba.