Taarifa ya Polisi imesema kuwa Nondo baada ya kutelekezwa na watu asiowajua katika eneo hilo alisimamisha Bodaboda na kumuelekeza amfikishe katika Ofisi za Chama chake Magomeni Jijini Dar es salaam ambapo alifikishwa hapo saa tano usiku na kuonana na viongozi wake kabla ya kupelekwa
Hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake
Taarifa za kutekwa kwa Nondo zilitolewa na Chama chake Jana jumapili na baadae Polisi walithibitisha kuwa wanamtafuta kiongozi huyo baada ya kuchukuliwa eneo la Stendi Mbezi Jijini Dar es salaam
Polisi wamesema wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo