Alhamisi , 20th Aug , 2015

Watu 6 wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti mkoani Njombe Wilayani Ludewa ikiwemo watano wa wa familia moja kufariki katika ajali na mtoto mmoja kuuawa kwa kuchomwa moto.

Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe Kamanda wa polisi wa mkoa huo Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa katika tukio la kwanza watu watano wa familia moja walifariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Lugalawa Wilayani Ludewa baada ya gari hiyo kuacha njia na kutumbukia katika mto.

Mtafungwa amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kutokana na mwendo kasi wa dereva wa gari hilo aliyetambulika kwa jina na Haron Haule alieshidwa kuimudu gari hiyo na kuiingiza mtoni na kupekelekea vifo vya watu hao papo hapo.

Katika tukio lingine limetokea katika kijiji cha Malimbuli, kata ya Manguti, wilayani Makete afisa mtendaji wa kijiji Alex Josephat, aligundua kuuawa kwa kuungua moto mtoto Joshua Seth (2) mkazi wa kijiji hicho na polisi inaendelea na uchunguzi juu ya tukio la kifo hicho.