Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mbeya Mjini Alhadji Mwangi Kundya.
Baadhi ya wanahabari waliojitokeza ni pamoja na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Ulimboka Mwakilili, Mwakilishi wa kampuni ya Business Times mkoani Mbeya Charles Mwakipesile, mwandishi wa habari wa kujitegemea Jackson Numbi na Shadrack Makombe mwandishi na mkurugenzi wa Generation F m ya jijini Mbeya.
Mwanamke pekee kati ya watia nia hao Fatuma Kaseka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Mbeya amewataka wana Mbeya wasirudie makosa huku Mwanachama Ashrey Hamimu akimuomba Aggrey Mwasanguti mwenye umri wa zaidi ya miaka 80 apumzike awapishe vijana ambapo naye alijibu hoja hiyo.
Sambwee Shitambala ni kamptein Mstaafu wa Jeshi la wananchi(JWTZ), Wakili na Mnec alijigamba kuwa yeye ni kiboko ya CHADEMA huku Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM Mkoa wa Mbeya Amani Kajuna akipiga magoti na amewaomba wanachama wampe ridhaa ya kuwatumikia.
Watia nia hao wameanza Julai, 20 kuzunguka katika kata zote 36 za jiji la Mbeya kujionesha kwa wanachama na kujinadi endapo watapewa ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM katika jimbo la Mbeya mjini.