Alhamisi , 11th Aug , 2022

Serikali kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimepokea ujumbe wa timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo, Maji na Mazingira ya Saudi Arabia

Ujumbe huo unaongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Ali Jabil Mwadini ili kufanya kikao shirikishi chenye lengo la kuchagiza uwekezaji kwa pande zote mbili katika sekta za Uvuvi, Kilimo na Sekta ya wanyama pori.

Akitofa ufafanuzi Kaimu Mkurugenzi Uhamasishaji Uwekezaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Revocatus Rasheli amesema lengo la  ujumbe huo ni kuja na mfumo shirikishi pamoja na  Taasisi za Serikali pamoja na Sekta Binafsi. 

Ujumbe huo umefika Tanzania kufuatia ziara ya Liberata Mulamula, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mwezi Machi 2022 alipokutana na uongozi wa Wizara ya Kilimo, Maji na Mazingira ya Saudi Arabia wakiafikiana kuzikutanisha timu hizo za  Wataalamu kutoka Wizara hiyo pamoja na Taasisi zilizopo chini yake watembelee Tanzania kuangalia maeneo ya uwekezaji na ushirikiano.

Wataalamu hao wamefika kuangalia mazingira na taratibu za usafirishaji wa mifugo hai ili kujiridhisha iwapo Tanzania inaweza kupewa kibali cha kuingiza mifugo hai katika soko la Saudi Arabia.

Aidha, wataalamu hao wataangalia fursa za uwekezaji katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi na namna ya kushirikiana katika sekta ya wanyama pori