Jumatatu , 13th Mar , 2023

Wafanyabiashara wa maduka mkoani Iringa wamesitisha mgomo wa kutokulipa tozo na kodi zilizo chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa baada ya machinga kuhamishwa na kupelekwa eneo la Mlandege ambalo wamepangiwa kufanya biashara zao.

Wafanyabiashara

Katibu wa jumuiya ya wafanyabaishara hao Kola Mtende amesema kuanzia sasa wataanza tena kulipa maduhuli ya Manispaa kama ilivyokuwa hapo awali baada ya zoezi la kuwaondoa wamachinga mbele ya maduka yao kufanikiwa

Miongoni mwa tozo zilizokuwa zimegomewa na wafanyabiashara hao ni tozo ya usafi, kodi ya leseni na kodi ya pango.

Ni takribani siku saba zimepita tangu lilipotolewa tamko na wafanyabishara hao wa mkoa wa Iringa kusitisha kulipa tozo zote zilizo chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, kutokana na kushindwa kuwapanga wa machinga katika maeneo waliyopangiwa na kupelekea mgongano wa maslahi kati ya makundi hayo mawili.