Baadhi ya wajasiriamali kati ya hao 450 walionufaika wamesema familia nyingi zinaingia katika mazingir magumu ya kiuchumi kutokana na wengi kukwama kupata mitaji ya kuanza biashara zao hivyo kuishukuru kamopuni hiyo kwa uwezeshaji huo.
Kwa upande wake meneja masoko kutoka kampuni hiyo amesema hiyo ni awamu ya tatu ambapo tayari huko nyuma wamewezesha mitaji vijana zaidi ya mia 600 lengo ikiwa kufungua fursa za kiuchumi kwa kila mjasiriamali kupitia kampeni hiyo ya chipska na coke.
Akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila mkuu wa wilaya ya kinondoni amewataka wadau wengine kuiga mfano huku akibainisha kwa kinondoni manispaa iko miradi mingi ambayo wadau wanaweza kujitokeza kushirikiana na serikali akiwataka watanzania waliopata uwezeshaji huo kuinuka kiuchumi.