Jumatano , 10th Jul , 2024

Wafanyabiashara katika Soko la Mazao la Kimataifa linaloingiza zaidi ya billion tatu lililopo katika Halmshauri ya mji Tunduma wametishia kugoma kwa kufunga biashara katika soko hilo kwa sababu za Halmashauri ya mji kushindwa kuwasikiliza na kutatua kero za miondombinu mibovu katika soko

Wakizungumzia kero za kukosekana kwa miundombinu ya Choo,kukosekana kwa taa pamoja na Ubovu wa mizani uliochukuwa muda mrefu bila kutatuliwa wananchi hao wamedai watafunga vyumba vya biashara na kuandamana mpaka Halmshauri itakapoenda kuwasikiliza na kutatua kero hizo.

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji huo amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kuomba radhi wananchi.

Naibu waziri wa Kilimo na Mbunge wa Jimbo la Tunduma Mhe DAVID SILINDE amewataka watumishi wa Halmshauri kupitia Mkurugenzi kutenga Muda wa kwenda Sokoni hapo kusiliza na kutatua kero za wananchi.