Alhamisi , 2nd Mar , 2023

 Wafanyabiashara katika soko la Machinga Complex wanaotengeneza Batiki wamesema moja ya changamoto kubwa inayowakabili ni upatikanaji wa mali ghafi kwa urahisi

Wakizungumza na EATV wamesema changamoto hiyo inachangia biashara zao kufanyika katika mazingira magumu 

Nao wafanyabiashara wenye biashara za kawaida wamesema kutokuwepo kwa uwiano sawa wa kibiashara ikiwemo kati ya wanaofanya biashara zao jumla wale waliopo eneo la chini la soko hilo nayo inachangia kuwarudisha nyuma kibiashara

Kwa upande wake mwenyekiti wa wamachinga katika soko hilo Said Mkupa amekiri kuwepo kwa changamoto hizo ambazo amesema zimekuwa zikifanyiwa kazi