Alhamisi , 15th Sep , 2022

Wafanyabiashara katika kituo cha Mabasi cha Dkt. John Pombe Magufuli Jijini Dar es Salaam, wamesema hivi sasa wanaunafuu wa gharama za upangaji katika jengo la kituo hicho kwakuwa gharama ya pango imepungua kutoka Sh. 160,000 hadi kufikia 90,000 kwa baadhi ya wafanyabiashara.

Eneo la biashara Stendi ya Dkt. Magufuli

Hatua hiyo inakuja baada ya kilio cha muda mrefu kutoka kwa wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katika kituo cha Mabasi cha Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu bei kubwa ya pango katika eneo la kupumzika abiria mabo ndio wateja wakubwa wa wafanyabiashara hao katika kituo hicho.

 Aidha, wafanyabiashara hao wamesema kuwa  hivi sasa wateja au abiria hawapatikani kwa wingi na kwamba abiria wengi hawafiki stendi na hii inaathiri hata wafanyabiashara walioko wengi na kwamba  wauzaji wa bidhaa wamekuwa wengi kuliko wanujuzi.

“Kwakweli tuneteseka sana kulipa kodi hapa, bei ya pango ilikuwa juu na sasa tunaishukuru serikali kwa kupunguza kodi katika kituo hiki. Mfano mwanzo nilikuwa ninalipa 160,000 kwa mwezi lakini sasa hivi ninalipa 90,000 kwa mwezi jambo ambalo linanipa unafuu. Changamoto imeibuka ni upungufu wa wateja, sasa hivi wateja hakuna kabisa tofauti na wiki mbili zolizopita"- Issa Suleiman, Mfanyabiashara JPM Stand.