
Sehemu ya Soko la Mtambani
Wakizungumza na Kurasa wameeleza kuwa wanalipa ushuru ila hakuna ukarabati unaofanyika kwa kipindi cha muda mrefu, hivyo soko haliendani na ushindani wa kisasa katika biashara.
Kuhusu usafi pia katika soko hilo, wamezungumzia changamoto ya gari la taka kupita sokoni hapo likiwa limejaa na wakati mwingine hukaa na uchafu hadi wiki Tatu.
"Tunalipa ushuru lakini hatuoni mabadiliko katika soko, wanapokumbuka pesa wakumbuke na marekebisho", amesema mmoja wa wafanyabiashara hao.