Jumatano , 16th Feb , 2022

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Sitholizwe Mdlalose, amesema kwamba Vodacom itahakikisha inaendeleza ushirikiano na mahusiano mazuri ya kibiashara yaliyopo na makampuni ya IPP Media.

Kushoto ni Meneja Matangazo wa East Africa TV na Radio Lydia Igarabuza na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Sitholizwe Mdlalose

Kauli hiyo ameitoa hii leo alipotembelea ofisi za makampuni hayo zilizopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuendelea kuboresha mahusiano, kujifunza namna yanavyofanya kazi zake kujua changamoto na fursa zaidi.

Aidha, ameyapongeza makampuni hayo kwa namna ambavyo yamewekeza katika uimarishaji wa mitambo yake ya kisasa pamoja na kuwa mbele zaidi katika ulimwengu wa kidigitali ambao kwa sasa ndio unaotumika zaidi.

Katika ziara hiyo ya IPP Media Bw. Mdlalose aliyeambatana na baadhi ya maafisa wa Vodacom Tanzania alitembelea Kampuni ya magazeti ya The Guardian, EATV na East Africa Radio, ITV/Radio One pamoja na Capital TV na Capital Radio.