
Mwenyekiti wa wabeba mizigo anayetambulika kwa jina la Mzanda amesema wameazimia kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga na kulima mboga mboga na matunda kwenye shamba lao la hekari 27 kwa njia ya umwagiliaji ili waweze kujikwamua kiuchumi
Vijana hao baada ya kuweka bayana azma yao kwa mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ameahidi kuwaunganisha na watoa mikopo wa manispaa ya Mpanda wawajengee kiwanda hicho na kuwapatia zana za umwagiliaji ili kikundi hicho kiwe cha mfano kwa vijana wengine wa Katavi huku pia akitoa agizo la siku Saba kwa watendaji wake.