
Inatarajiwa kuwa ifikapo mwaka 2025 mapipa ya kwanza ya mafuta yenye uwezo wa kufikia bilioni 1.4 yatasukumwa kutoka visima katika eneo la katikati ya magharibi.
Mamlaka ya Mafuta ya Uganda (PAU)imesema kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter kwamba, jumanne ya leo inakwenda kuwa hatua nyingine muhimu na kusogeza hatua karibu na mafuta ya kwanza kwa uzinduzi wa uchimbaji na uzalishaji wa mafutadeleo .
Rais Yoweri Museveni anatarajiwa kufanikisha hafla hiyo. Shughuli za uchimbaji mafuta huko Kingfisher zinaendeshwa na kampuni ya CNOOC ya China, huku eneo la Tilenga zikiendeshwa na kampuni ya Total Energie ya Ufaransa.